Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kusaidia mfumo rahisi wa umilikaji ardhi

FAO kusaidia mfumo rahisi wa umilikaji ardhi

Serikali ya Finland na shirika la chakula duniani FAO wamekubaliana kuzisaidia nchi mbalimbali kuanzisha mfumo endelevu na ulio rahisi wa umilikaji ardhi , ili kuimarisha udhibiti wa ardhi katika maeneo ya vijijini na mijini.

Mradi huo utakaogharimu dola milioni 2.4 utazisaidia nchi wanachama wa FAO kujaribu kuiga mfumo huo ambao ni wa gharama nafuu na tekinolojia rahisi kwa faida ya kuweka kumbukumbu zao za masuala ya ardhi.

Majaribio ya mradi huo yatafanyika Ghana, Nepal na Samoa. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu msaidizi wa FAO Alexander Muller mfumo mzuri na ulio wazi wa umiliki wa ardhi ni muhimu sana katika kuhakikisha usalama kwenye maeneo ya vijijini na mijini.