Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yanaendelea kutoa msaada Haiti

Mashirika ya UM yanaendelea kutoa msaada Haiti

Shirika la afya Duniani WHO inasema kuna haja kubwa na muhimu wa kupatikana manasi wanaohitajika kusaidia katika huduma za afya kwa wathiriwa wa tetemeko la ardhi.

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu UNFPA linasema zaidi ya wanawake elfu 63 wajawazito wamepatikana Port-au Prince pekee yake, elfu 7 kati yao wanatarajiwa kujifungua mnamo mwezi mmoja ujao. Karibu elfu 10 kati yao wanahitaji huduma za dharura kutokana na matatizo mbali mbali. Mmoja kati ya kila wanawake 47 wa Haiti wako hatarini ya kufariki wakati wa kujifungua. UNFPA imepeleka vifaa vya huduma za dharura ili kuweza kuwasaidia wanawake na haja zao.


Kwa upande wake WFP imeshaweza kuwasilisha rasheni milioni moja laki nne za chakula kwa karibu watu robo milioni. Idara hiyo ya chakula duniani inagawa ngano na mpunga kwa wanaoweza kupika. Na kuna zaidi ya watu laki moja wanapokea vifaa muhimu kila siku kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na washirika wake katika mji mkuu na maeneo mengine ya karibu