Haiti yakumbwa na tetemeko jingine

Haiti yakumbwa na tetemeko jingine

Haiti imekumbwa tena na tetemeko kubwa Ijumatano, na kutikisa majengo na kusababisha mtaharuku mkubwa, watu wakikimbia barabarani baada ya kushuhudia mtetemeko mkubwa ulosababisha maafa siku nane zilizopita.

Haikujulikana mara moja hasara zilizotokana na tetemeko la Jumatano lililokua na nguvu za 6 nukta moja, likiwa la 12 kukumba nchi hiyo mwezi huu wa Januari. Wakati huo huo, kufuatana na afisa wa cheo cha juu wa UM, hali ya usalama na kuratibu huduma za dharura inaendelea vizuri, lakini alikanusha ripoti za ghasia kuenea kote nchini wiki mmoja baada ya tetemeko linalodaiwa limesababisha takriban vifo vya watu laki mbili. Mjumbe maalum wa Katibu mkuu kwa ajili ya amani, Edmond Mulet aliwambia waandishi habari huko Port-au-Prince kwamba hali jumla ya usalama inazidi kua nzuri na alisuta kuenea kwa wizi wa ngawira.