Benki Kuu kutoa msaada zaidi wa dola milioni 100 kwa Haiti

Benki Kuu kutoa msaada zaidi wa dola milioni 100 kwa Haiti

Benki Kuu ya Dunia itatoa msaada zaidi wa dola milioni 100 kama mkopo wa dharura kusaidia kazi za uwokozi na kuikarabati taifa la Caribbean la Haiti.

Rais wa Benki Kuu Robert Zoellick amesema hili ni tukio la kushtusha sana na ni muhimu kwa jumuia ya kimataifa kuwasaidia wananchi wa Haiti katika wakati huu mgumu. Alisema Benki kuu ina changisha fedha nyingi za msaada na kupeleka timu za waatalamu kusaidia kutathmini hasara na haja za kuikarabati nchi. Bw Zoellick alisema dua zao ziko pamoja na wananchi wa Haiti, wafanyakazi wao na wenzao wa UM.

Mbali na msaada huo mpya Benki Kuu inatarajia kutumia uwezo wa miradi iliyoko huko tayari ikiwa ni pamoja na kuzingatia maswala ya elimu na maendeleo yatakaongozwa na jamii.