Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi vijiji vya millenia wapongeza kwa vita dhidi ya HIV/Ukimwi

Mradi vijiji vya millenia wapongeza kwa vita dhidi ya HIV/Ukimwi

Mshauri wa juu wa katibu mkuu amepongeza juhudi za mradi wa Vijiji wa Milenia MVP wa UNAIDS katika vita vya kupambana na ukimwi.

 Jeffery Sachs amesema UNAIDS imefanikiwa kuleta uzowefu wa kipekee wa kimataifa, uwongozi na mikakati kabambe katika vita dhidi ya HIV/UKimwi, ikiwa ni pamoja na juhudi za kuzuia mama kumwambukiza mtoto wake. Amesema mradi wa MVP umeweza kunganisha pamoja maendeleo ya maeneo ya mashambani, ikiwa ni pamoja na mifumo ya huduma za afya msingi katika vita dhidi ya umaskini, njaa na magonjwa. Kwa kuungana pamoja kati ya UNAIDS na MVP, Bw Sachs anasema kutaweza kuandaa na kutekeleza mfumo kabambe utakaopelekea kumaliza kabisa hali ya mama kumwambukiza mtoto wake, na mfano huo kuweza kutumiwa katika maeneo mengine ya Afrika na dunia. Sachs alisema hayo baada ya kutembelea pamoja na Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe moja wapo ya Vijiji vya Milenia huko Sauri, Magharibi ya Kenya kushuhudia wenyewe maendeleo yaliyopatikana katika vita dhidi ya umaskini, kuimarisha kilimo, elimu na afya, kwa ajili ya ukuwaji wa kudumu wa uchumi.