UNAIDS imetaka kuwepo na uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaishi na virusi vya HIV

6 Januari 2010

Mkuu wa Bodi la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe, ametoa wito wa kuwepo uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa mwaka huu wa 2010, mwaka ambao nchi mbalimbali zimeazimia kufikia malengo ya kimataifa ya kuzuia virusi vya ukimwi, kupata matibabu, huduma na msaada unaohitajika kwa wanaoishi na virusi hivyo.

"Tuhakikishe hakuna nchi inayomzuia mtu kuingia eti kwa sababu anaishi na ukimwi. Ubaguzi wa aina hiyo hauna nafasi katika dunia hii ya leo." amesema bwana. Sidibe. Kwa mujibu wa UNAIDS nchi zipatazo 57 zina vikwazo maalumu vya kuingia katika mipaka yake, kuishi na kupata uraia kwa walio na ukimwi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter