Mkutano wa Copenhagen umewakilisha fursa ya kuleta maisha bora kwa umma wa kimataifa, anasema mkuu wa IFRC

12 Disemba 2009

Bekele Geleta, KM wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) ametangaza taarifa maalumu ya taasisi yao kuhusu wasiwasi unaoambatana na maendeleo kwenye majadiliano ya Mkutano wa Copenhagen.

Alisema ni muhimu kwamba azimio la mwisho la mkutano litasisitiza juu ya wajibu wa Mataifa Wanachama kupunguza hatari inayochochewa na uharibifu wa mazingira duniani, na alitaka mataifa yajitayarishe kukabiliana na maafa kwa kuimarisha miradi kinga dhidi ya majanga haya ya kimaumbile. Mwelekeo unaotakikana kwa sasa, aliongeza kusema, ni ule utakaohakikisha kutakuwepo suluhu ya kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ili zisizuke tena, na pia kuhakikisha utaratibu uliopo umejaaliwa msaada wa fedha maridhawa za kukabiliana, kidharura, katika viwango vyote, vya kienyeji, kitaifa na kimataifa pindi maafa yatafumka.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud