Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti fupi kuhusu matukio ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen

Ripoti fupi kuhusu matukio ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen

KM Ban Ki-moon amenakiliwa akifuatilia, kwa ukaribu zaidi, hekaheka na harakati za kijumla kwenye Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya hewa, wakati majadiliano yakipamba na kuendelea miongoni mwa wajumbe wa kimataifa.

Hivi sasa, wawakilishi wanazingatia nyaraka kadha wa kadha zenye mapendekezo ya kuwasilisha itifaki ya kuridhisha, inayohitajika kudhibiti bora athari haribifu zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kabla ya Mawaziri wa Nchi Wanachama kuwasili Copenhagen mwisho wa wiki hii. Majadiliano ya sasa hivi yanalenga zaidi kwenye ahadi mpya za mataifa yenye maendeleo ya viwanda, chini ya Itifaki ya Kyoto na kusailia ushirikiano wa muda mrefu, chini ya Mkataba juu ya Udhibiti wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ikijumlisha masuala yanayohusu udhibiti wa athari za gesi chafu, marekibisho kwenye huduma za kiuchumi na kijamii, matumizi ya teknolojiya mpya na udhibiti wa uharibifu wa misitu. KM anaamini wapatanishi wanawajibika kusuluhisha mifarakano yao na kukamilisha, haraka, majadiliano, na kwa mafanikio, na alitilia mkazo kwamba pendekezo hilo ni deni wanaodaiwa na walimwengu.