Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaadhimisha Siku ya Haki za Binadamu

UM unaadhimisha Siku ya Haki za Binadamu

Tarehe ya leo, 10 Disemba (2009) inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Haki za Binadamu. Kwenye risala ya KM juu ya taadhima za siku hii, alihadharisha kwamba hakuna hata taifa moja duniani liliosalimika hivi sasa na tatizo la ubaguzi, tatizo linaloendelea kujiwasilisha kwenye mifumo na miundo aina kwa aina ya kijamii.

Alisema miongoni mwa mifumo ya ubaguzi iliojitokeza katika siku za karibuni kwenye baadhi ya nchi ni ule mfumo unaoambatana na sera mpya za chuki dhidi ya wageni. KM alionya kwamba ahadi upepo pekee za kuondosha tatizo hili, kutoka serikali za kimataifa, hazitoshi kukabiliana na uovu wa ubaguzi. Alizihimiza Nchi Wanachama kujumuika kupiga vita hali ya kutokuwa sawa na tofauti za fursa kwenye jamii zao ili kuyatekeleza maadili ya UM kama inavyotakiwa, na kukamilisha haki halali za kimsingi za binadamu kwa masilahi ya wote.