Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinzi amani wawili wauawa Darfur na shambulio la watu wasiotambuliwa

Walinzi amani wawili wauawa Darfur na shambulio la watu wasiotambuliwa

Vikosi vya Pamoja vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) vimetoa ripoti ya mwanzo, yenye kueleza wanajeshi wake wawili, walinzi amani wa kutoka Rwanda, waliuawa wakati walipokuwa wanateka maji kwenye eneo la Saraf Umra, Darfur Kaskazini.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, walinzi amani walishambuliwa na watu wenye silaha wasiotambuliwa. Kadhalika, wanajeshi kadha wengine waliripotiwa kujeruhiwa. Vikosi vya UNAMID vimewahamisha maiti na majeruhi kwenye mji wa El Fasher kwa mazishi na matibabu.