Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM adhamiria kumteua I. Gambari kuwa Mjumbe wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur

KM adhamiria kumteua I. Gambari kuwa Mjumbe wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur

KM amewajulisha wajumbe wa Baraza la Usalama leo hii ya kwamba anaazimu, baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kumteua Ibrahim Gambari wa Nigeria kuwa Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM/UA kwa Operesheni za Amani kwa Darfur, na kusimamia operesheni za vikosi vya pamoja vya UM-UA vya UNAMID, kuanzia tsarehe 01 Januari 2010.

Gambari atamrithi Rodolphe Adada wadhifa huo, baada ya kumaliza muda wake wa kazi. Balozi Gambari aliitumikia UM kwa sifa kuu na kwa muda mrefu sana, na katika miezi ya karibuni alikuwa ni Mshauri Maalumu wa KM juu ya Maafikiano ya Kimataifa kwa Iraq na kuhusu masuala mengine ya kisiasa. Vile vile Gambari alimsaidia KM kwenye utekelezaji wa madaraka aliodhaminiwa na Baraza la Usalama kusuluhisha suala la Myanmar.