Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC imerekibisha tena uamuzi wa kuachiwa kwa muda Bemba

ICC imerekibisha tena uamuzi wa kuachiwa kwa muda Bemba

Mapema Ijumatano Korti Ndogo ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), iliopo Hague, Uholanzi imebatilisha uamuzi wa siku za nyuma wa kumwachia Jean-Pierre Bemba kutoka kizuizini.

Mnamo mwezi Agosti, Korti Ndogo ya Mahakama Kuu ya ICC iliamua kumwachia, kwa sharti, kutoka kizuizini Bemba wakati akisubiri kesi, kitendo ambacho kilimfanyisha Mwendesha Mashitaka kutuma ombi maalumu liliopendekeza kwa Mahakama kusimamisha, halan, hukumu hiyo. Bemba alituhumiwa kushiriki kwenye makosa ya jinai ya vita na uhalifu dhidi ya utu, makosa yaliodaiwa yalifanyika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na sio ndani ya JKK, taifa ambalo Bemba ndio raia.