Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kupitisha mkataba wa kihistoria kudhibiti uvuvi haramu

FAO kupitisha mkataba wa kihistoria kudhibiti uvuvi haramu

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limepitisha mkataba mpya wenye lengo la kupiga marufuku vyombo vyote vya baharini na meli zilizoshiriki kwenye uvuvi haramu, kutoegesha kwenye bandari za Mataifa Wanachama.

Huu utakuwa mkataba wa awali wenye sheria ya kimataifa itakayotumiwa kudhibiti uvuvi haramu na wa siri. Maafikiano haya yatakuwa chombo cha sheria ya lazima ya kimataifa, pale nchi 25 zitakapouridhia mkataba. Hivi sasa nchi 11 wanachama wa FAO zimetia sahihi kuuridhia mkataba, ikijumlisha Angola, Brazil, Chile, pamoja na Kamisheni ya Ulaya, Indonesia, Iceland pamoja na Norway, Samoa, Sierra Leone, Marekani na Uruguay.