Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa mpya ya WHO kuhusu homa ya A/H1N1

Taarifa mpya ya WHO kuhusu homa ya A/H1N1

Hii leo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza taarifa mpya juu ya maendeleo, katika udhibiti bora wa homa ya mafua ya A/H1N1.

Ripoti imeeleza vijana wanaendelea kujumuisha jumla kubwa ya watu wanaoambukizwa na homa ya H1N1, na watoto wadogo pindi wanapatwa na virusi vya homa hiyo, hulazimika kulazwa hospitali. Bayana hii ilitangazwa na Kundi la Ushauri la Wataalamu (SAGE) juu ya tiba kinga na chanjo dhidi ya maradhi, wataalamu wanaoshauri WHO kwenye utekelezaji wa sera za chanjo, kimataifa. Baadhi ya watoto wanaopelekwa hospitali kutibiwa hulazimika kuwekwa kwenye vitengo vya wagonjwa wanaohitajia uangalizi shadidi, na vile vile wakati mwengine wanawake waja wazito nao pia huhitajia huduma kama hizo wanapopelekwa hospitali wanapopatwa na homa hiyo ya mafua. Wataalamu wa Kundi la Ushauri la SAGE wamependekeza watu wapatiwe chanjo zote mbili, kwa wakati mmoja, yaani ile chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya majira na dhidi ya janga la homa ya mafua ya H1N1 ili kuwahami na maambukizo.