Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa Kudhibiti Nimonia

Siku ya Kimataifa Kudhibiti Nimonia

Tarehe 02 Novemba, itaaadhimishwa, kwa mara ya kwanza na walimwengu, kuwa ni Siku ya Kimataifa Kudhibiti Homa ya Vichomi/Nimonia.

Kwa kuihishimu siku hii, Jumuiya ya Kimataifa Inayohudumia Chanjo na Kinga ya Maradhi, yaani Jumuiya ya GAVI, imejitayarisha kuchanja watoto milioni 130 katika nchi maskini, dhidi ya homa ya vichomi - ugonjwa ambao ni miongoni mwa maradhi yenye kusababisha vifo, kwa wingi, vya watoto wachanga duniani. Homa ya vichomi, ni aina ya maradhi yanayosababisha uvimbe wa mapafu, unaoletwa na maambukizo ya virusi, na ndio chanzo cha kilo kifo kati ya vifo vinne vinavyowapata watoto wachanga, na jumla ya vifo hivyo imekiuka vifo vinavyosababishwa na mchanganyiko wa maradhi ya UKIMWI/VVU, malaria na shurua. Kila mwaka nimonia inaua watoto wachanga milioni 1.8 chini ya umri wa miaka mitano. Licha ya kuwepo takwimu kama hizi za kushtusha, kimataifa, maradhi ya homa ya vichomi yamekosa kufadhiliwa na wahisani wa kimataifa msaada wa fedha zinazohitajika kuyadhibiti maradhi hayo kimataifa.