Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Zimbabwe imemnyima Mkariri wa Haki za Bindamu ruhusu ya kuingia nchini

Serikali ya Zimbabwe imemnyima Mkariri wa Haki za Bindamu ruhusu ya kuingia nchini

Serikali ya Zimbabwe imeripotiwa kuzuia ziara ya Manfred Nowak, mtaalamu wa UM juu ya masuala yanayohusu mateso, na vitendo vyengine visio vya kiutu vinavyodhalilisha hadhi ya ubinadamu.

Ofisi ya Kamisheni ya UM juu ya Haki za Binadamu imetangaza Nowak alipowasili Johannesburg, Afrika Kusini wiki hiii kuelekea Harare, aliarifiwa kwamba mwaliko wa ujumbe wake kuzuru Zimbabwe umeakhirishwa na Serikali mnamo tarehe 26 Oktoba (2009), kwenye taarifa iliosema Serikali "inahuzunika kushauri ya kuwa kutokana na mkutano wa Ushauri unaofanyika mjini Harare, sasa hivi, baina ya Serikali ya Muungano wa Taifa na wawakilishi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi kwa Kusini mwa Afrika (SADC), haitowezekana kumpokea Mtetezi Maalumu wa UM juu ya Haki za Binadamu kwa wakati huu." Nowak alisema anaukaribisha kidhati mpango wa juhudi za SADC, kurudisha utulivu Zimbabwe lakini, hata hivyo, alisisitiza "haamini mkutano wa Ushauri baina ya Serikali na SADC, utakaofanyika Alkhamisi, Oktoba 29, kuwa ndio kisingizio halali cha kufuta ziara yake ya ukaguzi, ya siku nane, katika Zimbabwe."