Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wairaqi, Waafghani na Wasomali waongoza jumla ya waomba hifadhi katika mataifa yenye maendeleo ya viwanda

Wairaqi, Waafghani na Wasomali waongoza jumla ya waomba hifadhi katika mataifa yenye maendeleo ya viwanda

Ripoti mpya iliotolewa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kuhusu maombi ya hifadhi ya kisiasa katika nchi zenye maendeleo ya viwanda, imebainisha ongezeko la asilimia 10 ya maombi hayo katika nusu ya mwanzo ya 2009, tukilinganisha na kipindi hicho hicho katika mwaka uliopita.