Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA imewasilisha maafikiano ya awali kuzingatiwa kuhusu nishati ya nyuklia kwa Iran

IAEA imewasilisha maafikiano ya awali kuzingatiwa kuhusu nishati ya nyuklia kwa Iran

Mohamed El Baradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) leo Ijumatano aliwaambia waandishi habari wa kimataifa kwamba baada ya siku mbili na nusu ya majadiliano mjini Vienna, taasisi yao imepitisha maafikiano ya awali kuhusu taratibu za kutumiwa kuisaidia Iran kupata nishati itakayotumiwa na kiwanda chao cha kiraia cha kufanyia utafiti wa matibabu.