Skip to main content

UNHCR inasema wahamiaji wa Angola waliofukuzwa JKK wanahitajia misaada ya dharura ya kuwavua na janga la njaa

UNHCR inasema wahamiaji wa Angola waliofukuzwa JKK wanahitajia misaada ya dharura ya kuwavua na janga la njaa

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo asubuhi aliwaarifu waandishi habari Geneva kwamba makumi elfu ya raia wa Angola waliofukuzwa kutoka JKK, ambao sasa wamewekwa kwenye vituo kadha vya makazi ya muda kwenye mji wa Mbanza-Congo, Angola kaskazini, wapo kwenye hali mbaya na wanahitajia misaada ya dharura kunusuru maisha. UNHCR ilipeleka Mbanza-Congo, katika mwisho wa wiki iliopita, ujumbe maalumu wa kutathminia mahitaji ya wahamiaji wa Angola waliofukuzwa kutoka JKK.