Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watahadharisha, uwekezaji mkubwa wa kilimo unatakikana 2050 kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu bilioni 9.1

UM watahadharisha, uwekezaji mkubwa wa kilimo unatakikana 2050 kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu bilioni 9.1

Wataalamu wa UM wameripoti kwenye makala ya majadiliano, iliochapishwa rasmi siku ya leo na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kwamba kunahitajika kufanyika uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya kilimo, kuhudumia chakula umma wa kimataifa kwa siku za baadaye, umma ambao ilisema unaendelea kuongezeka kwa kasi kuu.