Jumuiya ya kimataifa yalaani mauaji ya watumishi wa UM Islamabad

5 Oktoba 2009

Ijumatatu mchana, kwenye mji wa Islamabad, Pakistan watumishi watano wa UM wanaofanya kazi na Ofisi ya UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) waliuawa baada ya kufanyika shambulio la bomu la kujitolea mhanga kwenye jengo lao, tukio ambalo vile vile lilisababisha makorja ya majeruhi, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya kabisa na ambao hivi sasa wanapatiwa matibabu hospitali.

Kwenye mkutano na waandishi habari Geneva, KM wa UM, Ban Ki-moon alishtumu, kwa kauli kali, shambulio la Islamabad, na alisema kitendo hiki katili hakiwezi kutetetewa kwa njia yoyote. Alitilia mkazo kwamba licha ya tukio hilo, kazi zao hazitopwelewa na UM uatendelea kuhudumia misaada ya kiutu na kihali kwa raia milioni 2 waliong'olewa makazi nchini Pakistan. Miongoni mwa watu waliokufa, wanne walikuwa ni raia wa Pakistan na mtu wa tano aliyeuawa alikuwa mfanyakazi wa kutoka Iraq. Josette Sheeran, Mkurugenzi Mkuu wa WFP amesema kwenye risala yake ya kwamba waathirika wa shambulio walikuwa miongoni "mwa mashujaa wanaohudumia misaada ya kiutu waliojitolea kuweko katika msitari wa mbele wa kwenye vita dhidi ya njaa, hususan kwenye yale maeneo ambayo misaada ya WFP ndio huwa kamba ya kuokolea maisha kwa mamilioni ya watu muhitaji." Alisema shambulio la Ofisi za WFP Islamabad lilikuwa, sio msiba kwa shirika pekee, bali pia lilikuwa ni tukio la kusikitisha kwa jamii nzima inayohudumia misaada ya kiutu, na kwa ule umma wa kimataifa wenye njaa sugu ambao hutegemea misaada ya kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter