Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama kupendekeza UM uwe na Mjumbe Maalumu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsiya

Baraza la Usalama kupendekeza UM uwe na Mjumbe Maalumu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsiya

Baraza la Usalama lilkutana Ijumatano kuzingatia suala la hifadhi ya raia dhidi ya vitendo vyote vya kutumia mabavu na unyanyasji wa kijinsia, kwenye mazingira ya mapigano, hususan kwa raia wanawake na watoto wadogo.

Mkutano uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton. Baraza lilipitisha azimio, kwa kauli moja, kuridhia pendekezo la kuwapatia wanawake na watoto wadogo ulinzi imara dhidi ya matumizi ya nguvu na udhalilishaji. Kadhalika azimio limemtaka KM kuteua Mjumbe Maalumu atakayesaidia kuongoza jitihadi zilizo wazi, na kueleweka, kukabiliana na matumizi ya nguvu ya kijinsiya kwenye mazingira ya mapigano. Halkadhalika, KM alitakiwa kupeleka, haraka, timu ya wataalamu kufanya uchunguzi kwenye eneo fulani, pindi atapokea taarifa ya kwamba makosa ya jinai ya kijinsiya yamegundulikana kutendeka kwenye maeneo ya mapigano na vurugu.