Skip to main content

Mtetezi wa UM dhidi ya ufukara hanikiza kuzuru Zambia

Mtetezi wa UM dhidi ya ufukara hanikiza kuzuru Zambia

Magdalena Sepulveda, Mtaalamu Huru wa UM anayetetea haki za binadamu na umaskini uliovuka mipaka, anatarajiwa kuzuru Zambia kuanzia tarehe 20 mpaka 28 Agosti 2009, kufuatia mwaliko rasmi wa Serikali ya Zambia.

Bi Sepulveda amenakiliwa akisema ya kuwa lengo la ziara yake ni "kukusanya binafsi taarifa kuhusu hali ya ule umma unaosumbuliwa na ufukara wa hali ya juu" katika Zambia. Kwa mujibu wa taarifa ya Bi Sepulveda, Serikali ya Zambia sasa hivi inashiriki kwenye miradi kadha ya hifadhi ya jamii, mipango muhimu katika kupunguza umaskini uliovuka mipaka, miradi ambayo ataifanyia tathmini kwa mlingano sahihi wa kanuni za haki za binadamu. Magdalena Sepulveda ni mtetezi wa kwanza wa UM juu ya haki za binadamu kuzuru Zambia.