Maelfu ya raia wameng'olewa mastakimu na mashambulio mapya ya LRA katika JKK

Maelfu ya raia wameng'olewa mastakimu na mashambulio mapya ya LRA katika JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba muongezeko wa mashambulio ya kundi la waasi wa Uganda la LRA, kwenye Jimbo la Orientale, kaskazini mashariki katika JKK, yamesababisha raia 12,500 kung\'olewa makazi mwezi uliopita.