Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU inatafakaria masuala yahusuyo 'wanawake, amani na usalama'

BU inatafakaria masuala yahusuyo 'wanawake, amani na usalama'

Baraza la Usalama(BU) asubuhi, kwenye majadiliano ya hadhara, limezingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo kwenye utekelezaji wa mapendekezo ya azimio 1820 (2008), yanayoambatana na ulinzi wa wanawake kwenye mazingira ya mapigano.

Jamii ya kimataifa inakhofia zile sera za kuwalenga wanawake na kuwadhalilisha kimabavu, kwa makusudi, ambazo hutumiwa na wapiganaji, ni vitimbi vinavyohitajia kudhibitiwa haraka na jamii ya kimataifa, kwa sababu vinatengua haki za raia na kuhatarisha usalama na amani duniani. Ripoti ya KM ilielezea kwamba katika mizozo ya karibuni, na ile inayoendelea, wapiganaji wamegundulikana wakitumia utaratibu maalumu na mabavu kunajisi wanawake kihorera. Ripoti ya KM imependekeza vifungu 12 kwa Baraza la Usalama, vinavyotakiwa kupitishwa ili kukomesha udhalilishaji wa kijinsiya kwenye mazingira ya mapigano.