Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda imekamilisha uraisi wa BU kwa Julai

Uganda imekamilisha uraisi wa BU kwa Julai

Siku ya leo, tarehe 31 Julai 2009, ni siku ambayo Uganda inakamilisha uraisi wa kusimamia shughuli za Baraza la Usalama (BU) kwa mwezi huu.

Uraisi wa Baraza la Usalama hukabidhiwa kwa duru ya mwezi mmoja, miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Kuanzia Ijumamosi, tarehe mosi Agosti, uraisi wa duru wa Baraza la Usalama utakabidhiowa Uingereza. Balozi wa Uingereza katika UM anatumainiwa Ijumanne ijayo kutangaza ajenda ya shughuli za Baraza la Usalama kwa mwezi Agosti.