ICTR imehukumu kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

ICTR imehukumu kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) leo imemhukumu Tharcisse Renzaho, aliyekuwa kiranja wa Kigali-ville na pia Kanali wa Jeshi la Rwanda katika 1994, adhabu ya kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya halaiki, makosa ya vita na uhalifu dhidi ya utu.

Miongoni mwa makosa aliotuhumiwa nayo ilijumlisha jinai ya kuhamasisha mauaji ya raia wenye jadi za KiTutsi kwenye vizuizi vya barabarani, na kuendeleza karaha ya kujamii kimabavu wanawake na pia udhalilishaji wa kijinsia.