Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa mpya juu ya homa ya mafua ya A(H1N1)

Taarifa mpya juu ya homa ya mafua ya A(H1N1)

Shirika la Afya Duniani (WHO) leo limetangaza ripoti mpya kuhusu maambukizi ya homa ya mafua ya

A(H1N1) katika ulimwengu katika kipindi cha sasa.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, watu 55,867 wamesajiliwa rasmi, katika nchi mbalimbali za dunia kuambukizwa na homaya mafua ya H1N1 duniani, maambukizi ambayo pia yalisababisha vifo 230. Marekani imeripoti kuwa watu 21,000 ziada waliambukizwa na maradhi hayo nchini mwao, wakati Mexico ni taifa lenye kuongoza idadi ya watu waliofariki kutokana na homa ya H1N1, jumla ambayo ilithibitisha rasmi vifo 115 vya wagonjwa wa maradhi hayo.