Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raisi wa Gabon aombolezwa na KM Ban

Raisi wa Gabon aombolezwa na KM Ban

KM Ban Ki-moon ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, inayobainisha masikitiko yake makubwa juu ya kifo cha Raisi Omar Bongo Ondimba wa Gabon.

KM alisema Raisi Bongo "alisaidia pakubwa katika kuimarisha amani na utulivu, sio katika eneo la Afrika ya Kati pekee, bali pia katika maeneo mengine ya bara la Afrika." KM aliitumia aila ya Raisi Bongo mkono wa taazia, pamoja na Serikali na umma wa Gabon.