Hali ya usalama wa kigeugeu Kivu Kaskazini inaitia wasiwasi OCHA

5 Juni 2009

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama wa raia, ulioregarega Kivu Kaskazini, inaitia wasiwasi mkubwa wahudumia misaada ya kiutu waliopo katika JKK.

Kwa mujibu wa ripoti ilizopokea Ofisi ya OCHA karibuni imethibitika wazi kwamba mateso na udhalilishaji dhidi ya raia unandelea kufanywa na wafuasi wa kundi la waasi la FDLR, pamoja na baadhi ya wanajeshi wa taifa na pia makundi mengine ya wanamgambo ambao wamekutikana hushiriki hata kwenye vitendo karaha vya kujamii kihorera watoto wachanga. Iliripotiwa katika tarehe 20 Mei mtoto mchanga wa miaka mitatu alijamiiwa kihorera na wafuasi wa kundi la waasi la FDLR, mtoto ambaye alifariki njiani baadaye alipokuwa anapelekwa hospitali kutibiwa majeraha aliyoyapata kutokana na mateso hayo ya kijinsiya. Katika eneo la Minova, imeripotiwa asilimia 59 ya wanawake walisajiliwa hospitali kunajisiwa kimabavu katika kipindi cha baina ya tarehe 1 mpaka 23 Mei 2009. Kadhalika, mnamo mwezi April watu 49 walionajisiwa kimabavu walipelekwa hospitali kutibiwa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter