Skip to main content

ICC inazingatia ombi la kufuta kesi ya jinai ya vita katika JKK

ICC inazingatia ombi la kufuta kesi ya jinai ya vita katika JKK

Mapema wiki hii, Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), iliopo mjini Hague, Uholanzi ilianza kusikiliza hoja za wakili wa utetezi wa mtuhumiwa Germaine Katanga, aliyekuwa kamanda wa jeshi la mgambo katika JKK, hoja ambazo zilisisitiza ushahidi uliotolewa kuanzisha tena kesi dhidi ya mshitakiwa huyo haziwezi kutumiwa kuunganisha kesi mbili kisheria, na ushahidi huo usiruhusiwe wala kukubaliwa na Mahakama.