Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mizozo ya ajira duniani inasailiwa na ILO kwenye mkutano wa mwaka Geneva

Mizozo ya ajira duniani inasailiwa na ILO kwenye mkutano wa mwaka Geneva

Shirika la UM juu y Haki za Wafanyakazi (ILO) litaanzisha Mkutano wa Mwaka mjini Geneva hapo kesho, tarehe 03 Juni, ambapo majadiliano yake yataendelea hadi Juni 19.

Kikao hiki ni cha 98 na kitawakusanyisha wajumbe 4,000 wanaowakilisha serikali wanachama, mashirika ya waajiri na jumuiya za wafanyakazi, halkadhalika. Miongoni mwa masula yatakayozingatiwa mkutanoni ni pamoja na hatua za kuchukuliwa kipamoja kukabiliana na taathira zinazokithiri dhidi ya ajira, na masuala yanayohusu hifadhi za kijamii na ulimwengu wa wafanyakazi, nas kuzingatia athari haribifu zinachochewa na matatizo ya kiuchumi na kifedha, yaliotanda kwenye soko la kimataifa. Mkutano wa mwaka huu umeitishwa kusailia, kwa uangalizi mkubwa zaidi, taratibu za kuwahifadhi wafanyakazi, aila zao na shughuli za iktisadi dhidi ya madhara yanayopaliliwa na mizozo ya kiuchumi duniani, na pia kujaribu kuzingatia namna ya kufufua haraka shughuli za uchumi na ajira ili kukabiliana vyema na matatizo hayo.