Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya FARDC katika JKK vasaidiwa na MONUC kukabiliana vyema na waasi wa Kihutu nchini

Vikosi vya FARDC katika JKK vasaidiwa na MONUC kukabiliana vyema na waasi wa Kihutu nchini

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kushirikiana na vikosi vya taifa vya FARDC, kwenye operesheni maalumu za kuwafyeka kutoka mafichoni wapiganaji wanamgambo wa Kihutu, waliokuwa wakiendeleza vitendo vya ukatili wa aina kwa aina nchini dhidi ya raia.