Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe Malumu kwa Sudan ameingia wasiwasi juu ya usalama wa kusini

Mjumbe Malumu kwa Sudan ameingia wasiwasi juu ya usalama wa kusini

Kadhalika, baada ya ziara ya siku mbili Sudan Kusini, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, ambaye vile vile ni Mkuu wa Shirika la Ulinzi Amani la UM kwa Sudan Kusini (UNMIS) alisema ameingiwa wasiwasi juu ya kuharibika kwa hali ya utulivu kwenye eneo hilo mnamo miezi ya karibuni, kwa sababu ya mapigano ya kikabila yaliofumka kwenye majimbo ya Nile ya Juu na Jonglei.

Alisema idadi ya vifo vilivyosababishwa na vurugu na fujo Sudan Kusini katika kipindi hicho ilikiuka idadi ya vifo katika Darfur. Alibainisha kwamba mamia ya raia waliuawa karibuni kwenye mapigano katika Sudan Kusini, ikijumlisha wanawake na watoto wadogo, wakati maelfu ya raai waling'olewa makazi na kulazimika kuhamia maeneo mengine kutafuta hifadhi. Manmo mwanzo wa mwezi Mei, Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) iliripoti kwamba tangu Januari mwaka huu, karibu watu 1,000 waliuawa na Sudan Kusini, raia zaidi ya 100,000 waling'olewa makazi kwa sababu ya fujo kwenye majimbo saba ya Sudan Kusini.