Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Orodha fupi ya mikutano rasmi kwenye Makao Makuu

Orodha fupi ya mikutano rasmi kwenye Makao Makuu

Kwenye Makao Makuu ya UM, Ijumatatu ya leo, kumefanyika mkutano makhsusi wa Kamati Maalumu ya Kisiasa na Ufyekaji wa Ukoloni (au Kamati ya Nne). Vile vile wawakilishi wa kimataifa wamehudhuria kikao cha 17 cha Kamati juu ya Maendeleo ya Kusarifika.

Halkadhalika, kikao cha 31 cha Kamati Inayohusu Shughuli za Idara ya UM juu ya Mawasiliano kwa Umma, kimefunguliwa rasmi leo asubuhi, na pia kulifunguliwa rasmi kikao cha tatu cha Kamati ya Matayarisho juu ya Mkutano wa Mapitio wa 2010 kuhusu Wadaawa Walioidhinisha Mkataba wa Uzuiaji wa Uenezaji wa Silaha za Nyuklia Duniani.