Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa ya 13 ya WHO kuhusu homa ya A(H1N1) duniani

Taarifa ya 13 ya WHO kuhusu homa ya A(H1N1) duniani

Kwa mujibu wa takwimu mpya za WHO imeripotiwa nchi 20 zimethibitisha rasmi jumla ya wagonjwa 985 walioambukizwa na homa ya mafua ya A(H1N1).

Mexico imethibitisha watu 590 walipatwa na virusi vya homa mpya ya aina ya H1N1, iliosababisha pia vifo 25; wakati Marekani imethibitisha wagonjwa 226 walikutikana na homa hiyo, ikijumlisha kifo cha mtoto mdogo mmoja. Kanada imeripoti wagonjwa 85 walipatwa na homa, Uspeni wagonjwa 40, Uingereza watu 15 waliambukizwa na homa ya mafua, wakati Ujerumani waligundua wagonjwa 8 walipatwa na maradhi haya. Kadhalika, New Zealand iligundua watu 4 waliambukizwa homa ya H1N1; Israel, waliripoti wagonjwa 3 na El Salvador na Ufaransa wameripoti, kila mmoja, kugundua wagonjwa wawili waliambukizwa na homa nchini mwao. Mataifa mengine yaliogundua mgonjwa mmoja na homa ya mafua ya H1N1 katika maeneo yao ni kama ifuatavyo: Austria, Hong Kong, Uchina, Costa Rica, Colombia Denmark, Ireland, Utaliana, Uholanzi pamoja na Jamhuri ya Korea (Korea ya Kusini) na Uswiss.