Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP inazingatia sera mbadala kukomesha viumbe hai chafuzi (POP)

UNEP inazingatia sera mbadala kukomesha viumbe hai chafuzi (POP)

Paul Whylie, Ofisa Mratibu wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Stockholm dhidi ya Hatari ya Kuselelea kwa Viumbe Hai Chafuzi aliiambia Redio ya UM-Geneva kwamba walimwengu wanawajibika kuhakikisha afya ya wanadamu na mazingira hupata hifadhi ya pamoja dhidi ya athari hatari za vidudu chafuzi.

Alielezea kwenye mahojiano juu ya namna UNEP ilivyojishirikiasha katika maandalizi ya sera mpya, itakayochangisha kwenye zile juhudi za kukomesha matumizi yote ya dawa hatari ya DDT inayotumiwa kudhibiti vimelea vya malaria, hasa kwenye zile nchi zinazosumbuliwa na tatizo la maradhi haya, baada ya kugundulikana DDT huathiri pia afya ya wanadamu. UNEP sasa hivi inajaribu kuandaa mfumo mbadala ulio salama, wa kutumiwa kupiga vita vimelea vya malaria. Kwa mujibu wa UNEP, Viumbe Hai Chafuzi vyenye kudhuru afya ya wanadamu na mimea hujulikana kwa umaarufu kama Vichafuzi vya POP.  Mtaalamu wa taasisi hiyo Whylie alikumbusha kwamba virusi vya POP hukutikana kila mahalai - ndani ya majumba na katika anga, na vile vile kwenye maji ya kunywa na vyakula. Kadhalika alihadharisha kwamba viumbe chafuzi vya POP hukutikana, si kwenye dawa za kuuwa wadudu waharibifu pekee, bali pia kwenye makopo ya rangi, kutoka umajimaji unaosababishwa na hali ya joto, katika matransfoma na vile vile kwenye vitu vya plastiki. Hali kadhalika vijidudu hivi viharibifu huonekana kwenye takataka zinazotupwa kutoka mahospitali na kwenye makarkhana na viwanda. Whylie alisema ijapokuwa baadhi ya kemikali tulizozitaja zilichangisha kusaidia kuimarisha hali nzuri na ustawi wa maisha kwa wanadamu, hata hivyo dawa hizi pia zina hatari ya kudhuru afya ya wanadamu wanaokaribiana nazo.