Raia wa JKK wanaendelea kuhajiri vijijini kukhofu adhabu za waasi wa Kihutu

24 Aprili 2009

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limesema lina wahka juu ya usalama wa umma ulionaswa kwenye mazingira ya uhasama katika eneo la mashariki la JKK, ambapo hali inasemekana inaendelea kuharibika. Hali hiyo imesababisha makumi elfu ya raia kuhajiri makaz, kutafuta usalama na hifadhi, katika siku za karibuni.

"Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu kuharibika kwa hali ya maisha katike eneo la mashariki katika JKK, hali iliosababisha raia kukimbia makwao wakiogopa mashmabulio ya kulipa kisasi kutoka kundi la FDLR la waasi wa Kihutu." Alisema UNHCR inakadiria mashambulio ya waasi wa FDLR yanmesababisha watu 100,000 kung'olewa makazi katika miezi miwili iliopita. Alieleza kwamba katika kijiji cha Luofo, kilomita 170 kutoka Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu waasi wa FDLR walitangaza ripoti za kutishia kushambulia na kuadhibu wanakijiji wa eneo hilo. Lakini wanakijiji wa Luofo wamesema kuwa wao hawatohama makwao kwa sababu ya waasi, na wameomba hifadhi na misaada ya kiutu kutoka mashirika ya kimataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter