Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Taarifa ya KM iliotolewa Ijumatano usiku imeeleza kwa alifurahika kwa kuachiwa wale watu wanne waliotekwa nyara Afrika Magharibi miezi michache nyuma, ikijumlisha Mjumbe Maalumu wa KM kwa Niger, Robert Fowler pamoja na msaidizi wake Louis Guay, wote wawili wakiwa raia wa Kanada.

Alkhamisi alasiri Baraza la Usalama limezingatia shughuli za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Sudan Kusini (UNMIS). Baraza lilisikiza taarifa ya Ashraf Qazi, Mkuu wa UNMIS juu ya operesheni za UM kieneo. Vile vile kuhusu Sudan, UNHCR imeripoti kuwa, kuanzia mwazo wa mwaka huu, ilifanikiwa kuwasaidia wahamiaji 20,000 kuerejea makwao katika Sudan kutokea uhamishoni Uganda.

Mkutano wa Mapitio ya Maafikiano ya Durban juu ya Ubaguzi umemaliza majadiliano kwenye kikao cha wawakilishi wote Alkhamisi asubuhi, baada ya kusikiliza taarifa mbalimbali zilizoelezea hatari inayozushwa na mifumo ya kisasa ya ubaguzi. Mashirika kadha ya UM nayo pia vile vile yalishirki kwenye mijadala. Kwa mfano, Mjumbe wa Shirika la Haki za Wafanyakazi (ILO) alikumbusha kwenye risala yake ya kuwa ufunguo wa kuimarisha tabia ya kuhishimiana, kuvumiliana na kujumuisha utu miongoni mwa wafanyakazi, kote walipo ulimwenguni, upo kwenye mweleko wa maadili yanayohakikisha vitendo vya ubaguzi havitoruhusiwa kusitawi, abadan, kwenye mazingira ya ajira na kazi.

Mwakilishi wa Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) alielezea kwenye risala yake mbele ya Mkutano wa Mapitio ya Durban dhidi ya Ubaguzi mchango muhimu wa taasisi hii ya kimataifa katika kukomesha zile nadharia za sayansi ya uwongo, zenye kujigamba, kwa kiburi, ubora wa kikabila dhidi ya tamaduni nyenginezo zilizo tofauti.