Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtetezi wa mazeruzeru Tanzania ahimiza UM usaidie uimarishaji wa haki zao kimataifa

Mtetezi wa mazeruzeru Tanzania ahimiza UM usaidie uimarishaji wa haki zao kimataifa

Kwenye wiki ya tarehe 20 mpaka 24 Aprili wajumbe kadha wa kadha kutoka Mataifa Wanachama wa UM walikusanyika mjini Geneva, Uswiss kuhudhuria Mkutano wa Maafikiano ya Durban kwa makusudio ya kutathminia, na pia kuharakisha, utekelezaji wa mapendekezo yaliopitishwa na kikao cha awali cha 2001, katika Durban dhidi ya ubaguzi.

Lengo la Mkutano wa Dunia Kupinga Ubaguzi, uliofanyika Durban, Afrika Kusini 2001 lilikuwa ni kuhifadhi na kuyafanya bora maisha ya mamilioni ya umma wa kimataifa wanaoteseka na janga la ubaguzi la aina moja au nyengine. Moja ya tatizo la ubaguzi liliosailiwa ambalo huathiri fungu kubwa la wanadamu, katika baadhi ya mataifa, ni lile linalohusiana na tabia karaha ya kusubu, kutenga na kuwatesa ndugu zetu walio mazeruzeru. Mwaklilishi wa Bunge kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayeitwa Al Shaymaa John Kwegyir ni mmoja wajumbe aliye zeruzeru na aliyehudhuria Mkutano wa Geneva wa Mapitio dhidi ya Ubaguzi. Mtayarishaji vipindi wa Redio ya UM Geneva, Patrick Maigua, alipata fursa ya kuzungumza naye kuhusu ubaguzi wa mazeruzeru na hatua zinazotakikana kuchukuliwa kukomesha tatizo hili.

Sikiliza mazungumzo kamilio kutoka idhaa ya mtandao.