Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza tume ya uchunguzi juu ya ukiukaji sheria za kiutu Ghaza

3 Aprili 2009

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limetangaza kumteua Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini kuongoza ile tume huru ya kuchunguza ukweli kuhusu ukiukaji wa sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu, na uvunjaji wa haki za kiutu, uliofanyika wakati mgogoro wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza ulipopamba mnamo miezi kichache iliopita.

Wajumbe wengine wa tume hiyo wanajumlisha Profesa Christine Chinkin wa Chuo cha London cha Uchumi na Taaluma ya Siasa (London School of Economics and Political Science) katika Chuo Kikuu cha London; pamoja na (Bi) Hina Jilani, Wakili katika Mahakama Kuu ya Pakistan, ambaye pia alikuwa Mjumbe Maalumu wa KM Kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu, na Kanali mstaafu Desmond Travers, aliye mjumbe wa Bodi la Wakurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (IICI).

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter