Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu saba wapoteza maisha katika ajali nje pwani ya Yemen.

Watu saba wapoteza maisha katika ajali nje pwani ya Yemen.

Kiasi ya wahamiaji saba wa Kiafrika walizama na kufariki mwishoni mwa wiki wakati meli ya biashara ya magendo walokua wanasafiria ilipozama muda mfupi tu baada ya kutia n\'ganga kwenye bandari ya Aden huko Yemen.

Shirika la UM la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, liliripotri ajali hiyo na kueleza kwamba watu wengine 85 walinusurika kutokana na juhudi za uwokozi za maafisa wa mji huo na manuari ya jeshi la Ufaransa. Tukiyo lilitokea Jumamosi wakati maabiria walipojaribu kushuka kwa pamoja boti iliyokua imevutwa na meli ya kifaransa baada ya kupatikana katika Ghuba ya Aden ikielea na matatizo na kuanza kujaa maji.