Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum apongeza mkataba na waasi huko DRC

Mjumbe maalum apongeza mkataba na waasi huko DRC

Mjumbe maalum wa UM huko JKK amesifu makubaliano yaliyotiwa sahihi Ijumatatu kati ya serekali ya Kinshasa na kundi la waasi lililokua likiendesha mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya nchi mwaka jana.

Mwakilishi wa KM Alan Doss, amesema mkataba huo unaleta afweni kwa wakazi wa mashariki ya DRC , hasa wanawake na watoto ambao kwa muda mrefu wamekua waathiriwa wa vita, kukimbia makazi yao, na ubakaji. Aliongeza kusema kwamba ikiwa makubaliano hayo kati ya serekali na kundi la CNDP yataheshimiwa basi yatakua na manufaa makubwa kabisa kwa maisha ya watu wa majimbo mawili ya Kivu Kaskazini na Kusini. Kiasi ya watu elfu 250 walikimbia makazi yao kutokana na mapigano katika majimbo hayo mwaka jana. Wapatanishi maalum wa KM kwa maeneo ya Maziwa Makuu marais wa zamani Olusegun Obasanjo na Benjamin Mkapa walihudhuria sherehe za kutia saini mkataba huo.