Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kuwachanja watoto Rwanda

UNICEF kuwachanja watoto Rwanda

Wizara ya afya ya Rwanda ikisaidiwa na shirika la Watoto la UM, UNICEF, imezindua kampeni ya pili ya wiki moja, kuwahi kufanywa nchini humo ya kuwapatia kinga watoto na kina mama kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa kwa urahisi.

 Licha ya takwimu zinazoeleza kupunguka kwa idadi ya watoto wanaofariki kutokana na magonjwa kama kuharisha na malaria, lakini kuna watoto elfu 30 kila mwaka wanafariki kabla ya kutimia mwaka mmoja. Mnamo kampeni hiyo ya wiki nzima karibu watoto milioni moja na nusu chini ya umri wa miaka mitano watapatiwa chanjo, dawa ya minyo na tembe za vitamin A. Na watoto wengine milioni 3 wa shule chini ya umri wa miaka 16 watapewa temba za kuzuia magonjwa ya tumbo, na zaidi ya hayo wanawake wajawazito laki tatu watapigwa shindano ya kuzuia pepopunda.