Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wapanda Kilimanjaro kuhamasisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Vijana wapanda Kilimanjaro kuhamasisha athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Tume ya vijana 10 kutoka Kenya, Tanzania na Ghana wamefikia kilele cha Mlima Kilimanjaro huko Tanzania ikiwa ni sehemu ya kampeni ya UM ya kuhamasisha athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

Vijana hao wa kiafrika walowasili kwenye kilele cha Kilimanjaro Alhamisi iliyopita wakiadhimisha mwaka wanne wa Mradi wa Kupanda Mlima Kilimanjaro unaongozwa na shirika lisilo la kiserekali huko Nairobi kwa ushirikiano na UM. Walipowasili huko juu walimpigia simu KM Ban Ki-moon ambae binafsi alipita kwa ndege kwenye mlima huo wiki iliyopita na kumweleza kwamba maji na theluji imepunguka kwenye mlima huo.