Liberia yazindua mpango wa kitaifa kwa ajili ya wanawake amani na usalama

Liberia yazindua mpango wa kitaifa kwa ajili ya wanawake amani na usalama

Tarehe 8 March ilikua siku kuu ya wanawake duniani kukiweko na sherehe mbali mbali katika kila pembe ya dunia, ili kuhamasisha haki na maendeleo ya wanawake.

Huko Liberia Rais Ellen Johnson-Sirleaf, alizindua mpango wa kitaifa wa kuchukuliwa hatua, unaoungwa mkono na UM wenye lengo la kuimarisha usawa wa kijinsia, amani ya kudumu na usalama. Mpango ulizinduliwa kama sehemu ya warsha ya Kimataifa juu ya kuwawezesha wanawake, maendeleo ya uwongozi, pamoja na amani na usalama wa kimataifa inayofanyika huko Monrovia, kuanzia tarehe 7 hadi 10 mwezi huu. Kiasi ya wakuu 20 wa serekali wa hivi sasa na wa zamani na wajumbe 50 wa UM wanahudhuria warsha hiyo inayojaribu kutafuta njia za kuwawezesha wanawake kua viongozi hodari kwa kuwaunganisha pamoja na wenzao kutoka sehemu nyenginezo za dunia.