Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Obama kukutana Washington wiki hii

Ban na Obama kukutana Washington wiki hii

KM Ban Ki-moon atakutana na Rais Barack Obama wa Marekani huko Washington kwa mazungumzo juu ya masuala mbali mbali ikiwemo mzozo wa kiuchumi duniani, Sudan, Afghanistan na Mashariki ya Kati.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa KM inaeleza kwamba viongozi hao wawili wanatazamiwa pia kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa, haki za binadamu, mageuzi ya UM na uhusiano kati ya UM na Marekani. Akiwa Washington kwa siku mbili kuanzia Ijumatano KB atakua na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Njee Bi Hillary Clinton na wajumbe wa kamati za bunge juu ya masuala ya kigeni. Bw Ban atawasili Washington kutokea Haiti ambako anafuatana na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambako wamekwenda kutathmini na kuhamasisha haja ya kutoa msaada kwa wananchi na serekali ya taifa hilo fukara la Caribean.