Mahakama maalumu ya Sierra Leone yawapata na hatia viongozi watatu wa waasi

27 Februari 2009

Watu watatu walokiongoza kundi la kikatili la waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone wamepatikana na hatia ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu na mahakama maalum inayoungwa mkono na UM huko Freetown.

Mahakama hiyo maalum iliwapata na hatia viongozi wa zamani wa kundi la RUF Issa Hassan Sesay na Morris Kallon kwa makosa 16 kati ya 18, ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto kua wanajeshi, na ndoa za nguvu. Mkuu wa usalama wa RUF Augustine Gbao alipatikana na hatia 14. Hukumu zao zitatolewa katika wiki chache zijazo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter