Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ametoa mwito wa kukomesha mapigano na ghasia kote Afrika

KM ametoa mwito wa kukomesha mapigano na ghasia kote Afrika

Akiendelea na ziara yake ya Afrika, KM Ban Ki-moon alikutana Alhamisi na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania mjini Dar es Salaam, kwa mazungumzo juu ya masuala mbali mabli, kuanzia uchaguzi ujao nchini humo, mizozo ya kikanda na janga la uchumi duniani.

Viongozi hao wawili walizungumzia pia juu ya hali huko Burundi, Zimbabwe, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika mkutano mwengine tofuati ulongozwa na rais Kikwete, Bw Ban alikutana na rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyemuarifu juu ya mazungumzo ya Nairobi yenye lengo la kuleta amani huko JKK. Bw Mkapa ni mwenyekiti mwenza pamoja na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kaika mazungumzo hayo ya Nairobi. Hiyo jana KM aliwahutubia mabalozi wa kigeni, wasomi na wajumbe wa vyombo vya habari, na kutoa mwito kwa nchi za kiafrika kutumia uwezo na ujuzi wao katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia

Mara nyingi Afrika inaonekana kua bara la maafa na migogoro, jambo na hisi si kweli, mara nyingi nina wambia wenzangu kua Afrika ni ardhi ya matumaini, utajiri na uwezo mkubwa. Ni suala tu la wakati na nia dhati wakati uwezo na utajiri utakapo tumiwa na hapo ndipo nguvu za Afrika zitakapoonekana

Bw. Ban aliwataka viongozi wa kiafrika kusonga mbele katika maendeleo ya elimu, juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na vita dhidi ya VVU na UKIMWI. Baada ya Tanzania KM ataelekea JKK, Rwanda na hatimae Misri.