Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya Wasomali elfu 40 walokimbia makazi yao warudi Mogadishu licha ya mapigano

Zaidi ya Wasomali elfu 40 walokimbia makazi yao warudi Mogadishu licha ya mapigano

Shirika la UM la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, linaripoti kwamba zaidi ya watu elfu 40 walokimbia makazi yao IDP\'s wamerudi katika mji mkuu wa Mogadishu huko Somalia licha ya mapigano makali kutokea huko katika kipindi cha wiki sita zilizopita.

Msemaji wa UNHCR William Spindler amesema mapigano hayo yamesababisha vifo na majeruhi wengi na shirika hilo linasema linatathmini kiwango cha walokimbia kutokana na vita hivyo vipya. Kuna zaidi ya wa Somali milioni 1 laki tatu walokimbia kutoka makazi yao na kuishi ndani ya nchi, wakati mwaka jana pekee kuna laki moja walokimbia hadi nchi jirani.